Saturday, 21 November 2015

JUA UWEZO ULIONAO ILI UFANIKIWE



JUA UWEZO ULIONAO ILI UFANIKIWE


Na Samuel Sasali


Usikomalie kufanya jambo ambalo hujapewa neema ya kufanya utabaki unapoteza muda, unapoteza nguvu na unapoteza hata mvuto kwa kung’ang’ania kufanya. Kuna watu nimewahi ona waliwahi ng’ang’aniza kufanya mambo ya kakwama, lakini kazi ile ile akaja akafanya mtu mwingine kwa wepesi sana mpaka watu wakauliza “ulikuwa wapi saa zote”?. 




Mara zote nimekuwa nikisema maji huwa hayajitahidi kuserereka kwenye bonde ama Moto huwa haujitahidi kuunguza kwa sababu ndio kazi yake itakuwa ni ajabu sana Moto ukatamani kufanya kazi ya barafu, au siku miguu ikatamani kufanya kazi ya macho. Jicho huwa halifundishwi kuona ila linakatazwa kutazama ukiruhusu tu kuona jicho linaweza vuka mpaka katika kutazama.


 Nini ambacho kwenye maisha unakifanya pasipo kujitahidi?Watu huwa wanashangaa sana ninapata wapi uwezo wa kuandika makala ndefu kila ninapopata nafasi wakati mimi nawashangaa wao wanashindwajwe kuandika kitu kirefu. Jambo lile lile lakini neema tofauti. Wingi wa Nywele hausababishi kichwa kilemewe na Uzito.


Gari kama haujui namna ya kuliwasha haimaanishi ni bovu ila wewe ndio huna ufahamu wa kujua pa kuwashia. Mara nyingi sana tumekuwa wepesi wa kulaumu yale tunayoyafanya kwa kuonekana kama ni magumu kwetu..utasikia watu wanasema Shule ngumu sana aiseee…..ama mwingine anasema kuwahi wahi ofisini asubuhi hawezi, kuna mwingine yeye bila kufanya kazi huku anawasemesha wengine hajisikii raha, ajabu ni kwamba anafanya kazi huku anaongea sasa jaribisha wewe ambae huna huo uwezo lazima kimoja kisimame kupisha kingine, either Story ziendelee Kazi isimame ama Kazi ziende bila story.


Ukiona jambo linakutumia nguvu sanaaa kulifanya litokee tafuta sababu inawezekana unalazimisha groves la kwenye ngumi la mikononi uvae miguuni. Tairi la Trekta nyuma huwa halikai mbele hata kama Trekta limeharibika Porini.
Wingi wa Nywele haumaanishi Kichwa Kitalemewa.


Sasalithebloger


No comments:

Post a Comment