Thursday 1 October 2015

TAFUTA VITU VISIVYOONEKANA ILI UFANIKIWE

TAFUTA VITU VISIVYOONEKANA ILI UFANIKIWE

Na Ferdinand Shayo



Watu wengi huvutiwa na kupenda vitu vinavyoonekana kwa macho lakini wamesahau kuwa kuna vitu visivyoonekana kwa urahisi na vina thamani kubwa kuliko vile vinavyoonekana kwa urahisi mfano wa madini ya dhahabu ama Tanzanite.


Kadhalika ndani ya mtu kuna vitu vya thamani visivyoonekana wazi navyo ni vya thamani kuliko hata vile vinavyoonekana.

Kila binadamu ana kitu cha thamani ambacho badohajakitumia unaweza kuwa uwezo wa ajabu,vipaji na ubunifu ama uvumbuzi wa kitu.Vitu hivyo vina thamani kuliko vile vinavyoonekana.

Ukitazama picha ya maisha yako uliyopewa na Mungu (future) utagundua kuna vitu vingi unavyo lakini vichache tu ndo unavyo unavimiliki katika uhalisia wa maisha.

Kazi kubwa uliyonayo ni kufanya vile ambavyo hauna vitoke nje usibaki tu kujisifu kuwa vikondani yako au kujisifu kwa vile ulivyonavyo ambavyo vinaonekana wakati kuna vingi vya thamani visivyoonekana ambavyo hauna.

Wakati watu wengi wanagombania na kushindania vitu vinavyoonekana wanasahau kuna vitu vya thamani visivyoonekana kirahisi mfano wa Dhahabu.

Usiridhike na kile ulichonacho jitazame kwa macho ya ndani utaona kuwa vilivyoko ndani yako ni vingi ila ulivyonavyo mkononi ambavyo unaweza kuvishika ni vichache.

Viko vitu ambavyo unastahili kuwa navyo katika maisha na viko ambavyounastahili kuvifanya vinaweza kuwa kusudi la maisha yako chakushangaza umeridhikana vile ulivyonavyo na unavyovifanya jambo ambalo ni hatari huweza kutengeneza udumavu katika maisha.

Wengine wanavyo vitu kwa ajili ya watu lakini wameendelea kuishi kwa ubinafsi wanaishi kwa ajili yao wenyewe na si kwa ajili ya watu kama walivyokusudiwa katika maisha yao,hilo linatosha kuua uwezo,kipaji na talanta walizopewa na Mungu.

Yako mambo makubwa duniani ambayo bado hayajatokea yakaonekana kwa macho ziko ndani ya watu .Mambo hayo yako ndani yako wewe kazi yako ni kuruhusu yatokee kwenye uhalisia.

Ziko teknolojia ambazo bado hazijaingia duniani ziko ndani ya watu,ziko nyimbo ambazo hazijawahi kuimbwa ,vitabu ambavyo havijawahi kuandikwa ,dawa za magonjwa ambazo hazijawahi kugunduliwa zote ziko ndani ya watu.

Inawezekana zikondani yako ,Hakuna mtu yeyote mbali na wewe anayejua kitu kilichoko ndani yako isipokua wewe mwenyewe na Aliyekuumba.

Kama unashangaa kuona mambo makubwa na ya ajabu ,mambo mazuri,majengo makubwa na marefu bado hujashangaa vizuri kuna vitu vikubwa vya ajabu,vya tofauti na vya thamani ndani ya watu wakiamua kuviachilia nje ,Utashangaa na kupigwa na butwaa kila unapotembea kwa mambo utakayoyaona.

Si kweli kwamba dunia itajaa kila mtu akiamua kuachilia vitu vilivyoko ndani yake ,Ukweli ni kwamba Bado kuna nafasi spesho duniani iliyotengwa kwa ajili ya wewe kuachilia kile kilichoko ndani yako mfano wa sehemu maalumu zilizotengwa kwa ajili ya kuku kutaga mayai kutamia na kutotoa vifaranga.

Iwapo utaachilia kitu kilichoko ndani yako kizazi kijacho kikija kitakuta nafasi iliyoachwa wazi kwasababu hukutumia vizuri uwezo ,vipaji ulivyonavyo kwa faida yako na vizazi vijavyo.


ferdinandshayo@gmail.com

No comments:

Post a Comment