ACHA KUOTA NDOTO TIMIZA NDOTO ZAKO
Na
Samuel Sasali
Kati ya
changamoto kubwa tulizonazo kwenye kizazi chetu ni kuamua kufanya na kusimamia
kile unachoamua kufanya.
Wengi wetu
ni kweli tuna ndoto na wengine wana ndoto kubwa sana. Wengi wetu tuna mikakati
mingi,kila siku tunasema "wacha nijipange, wiki ijayo
naanza"....mwingine anaapa na kuapa kuwa mwezi ujao anaanza rasmi lakini
wapi mambo yale yale unadhani kwamba hataki kutimiza ndoto la hasha sababu
anayo uwezo anao unadhani kinakosekana nini?NIA ndiyo inayokosekana katika
kutimiza ndoto zetu.
Nia ya
kutenda na kutimiza ndoto inahitaji nidhamu ya hali ya juu kuweza kutimizwa.
Muulize mtu yeyote ambaye ambaye alitimiza ndoto bila kuwa na nidhamu.
Nia haipimwi
kwa mikakati ila inapimwa kwa utekelezaji. Wengi wetu tuna Diarly za kuandikia
tuna mikakati ya kimaandishi lakini Utashi wa kutimiza matakwa na mikakati na
Nidhamu ya kutimiza ndoto ndiyo changamoto kubwa.
Dhamira ya
utekelezaji ikiwa chini kuliko mihemko ya kutaka kuonekana na watu kuwa nawe
una ndoto ya kutimiza hupelekea kubaki vile vile katika maisha yako.
Ni lazima
utengeneze mazingira ya kuinua nia yako ya ndani kwa njia mbalimbali. Inua nia
yako ya kutimiza ndoto kwa kuuliza watu, kusoma vitabu, kama unaamini katika
Mungu fanya maombi, watembelee wanaotimiza ndoto kama ya kwako, tafuta taarifa
za kutosha kuhusiana na ndoto yako.
No comments:
Post a Comment