Thursday 1 October 2015

Usiuchekee Uamuzi Utakaokugharimu Baadae.

Na Samuel Sasali

Ugumu ama wepesi wa maamuzi hutegemea sana uwezo wa muamuaji katika jambo lililo mbele yake. Na ugumu ama wepesi haupimwi kijinsia wala kiumri wala kinamna yoyote ila kwa uwezo ambao kila mtu amejaaliwa na Mungu.

Tuko hiVi tuliVyo kutokana na maamuzi mbalimbali ambayo tuliwahi kuamua. Nyumba unayoishi, biashara unayofanya kila uliCho naCho ni matokeo ya maamuzi uliyowahi amua wakati fulani kwenye maisha. Kuna maamuzi ambayo wakati mwingine tumekuwa tukiamua huku tukijua fika maamuzi hayo yatatugharimu lakini pengine tumeamua kufanya tukijiaminisha kuwa mabaya yanaweza yasitokee.


Wanandoa wanapoamua kwenda kwenye miChepuko huwa wanajua fika siku mambo yao ya kuChepuka yatakapojulikana itawagharimu uaminifu, wakati mwingine magonjwa na mambo kadha wa kadha lakini unakuta mtu anaamua kwenda kwenye miChepuko.

Kuna watu ambao wao huku wakijua fika ngono zembe ni hatarishi lakini unakuta waathirika wakubwa wakiwa Vijana wanajihusisha na maamuzi ambayo wanajua mwisho wa siku watakuwa na majuto.

Unaweza kuta mtu anaamua kugusa umeme huku akiwa na maji maji akiamini ataChomeka harakaharaka pasi yake ama TV mwisho wa siku anapoteza. UsiuChekee uamuzi Utakaokugharimu baadae.

Wakati mwingine huwa tunadhani maamuzi tunayoyafanya ni yakwetu peke yetu na tunasahau kuwa maamuzi hayo hugharimu familia zetu, ndugu zetu na mengine huaCha majeraha mengi kwenye mioyo yetu.

Unapoamua kuchukua maamuzi ambayo yanaweza kukugharimu wewe na familia yako ni heri wakati wa kuchukua maamuzi hayo ukawajunuisha na watu wa nyumbani kwako. Inawezekana maamuzi tunayoyafanya gharama yake ikawa mzigo kwa familia pale sisi tunapokuwa tumetangulia mbele za haki.

UsiuChekee uamuzi utakaokugharimu. Chukua muda tafakari

samsasali.blogspot.com

No comments:

Post a Comment