JINSI YA KUTENGENEZA MTAZAMO CHANYA UTAKAOKUFIKISHA KWENYE MAFANIKIO
Na Ferdinand Shayo
Mafanikio haimaanishi kukosekana kwa kushindwa bali ni kushinda vita ila sio kwa kila pambano.Katika maisha ya kila siku unaweza ukawa umeshakutana ama kuwaona watu wanaoshangaa maisha yao,wanashangaa kwasababu walikubali majaliwa
yalipowapeleka.Wachache sana wanaofanikiwa kwa majaliwa
lakini wengi wanapata shida kwenye maisha kwasababu ya hili.
Kwanza kabisa tengeneza
ama panga vitu vifuatavyo (Action plan) inayojikita kwenye mambo
makuu matatu:1.Nini hasa unataka kukifikia (lengo) 2.Na unahitaji
lengo lako litimie lini? 3.Unafikiri utalifikiaje hilo lengo
unaangalia mikakati uliyoiweka,njia utakazotumia kufikia lengo
lako,mbinu na vifaa ili kuweza kufanikisha malengo yako katika
maisha.
Suala la Mafanikio katika
maisha linaanzia kwenye mitazamo na fikra zilizoko ndani ya mtu,kile
kilichoko ndani ya mtu ndicho kitakachomhesabia mafanikio
yake.Mtizamo peke yake ndo msingi wa maisha ambapo mtizamo unachukua
asilimia 64 ya nafasi katika maisha ya mtu.Ni vyema tukajifunza
kutengeneza mitazamo chanya ili tuweze kufanikiwa na njia mojawapo ya
kutengeneza ni kufikiria mema tu na kuacha kufikiria mabaya
kwasababu siri ya kushinda katika maisha ni
kuondoa fikra za kushindwa.
Mfano mtu mmoja alikuwa
akiishi kwa kuuza mapulizo.Alifanya baishara yake hiyo kwa muda
mrefu, na kupata mafanikio mazuri sana hasa kiuchumi. Baada ya watu
wengi kuzuka waliofanya biashara kama yakwake, uchumi wake ukaanza
kupormoka siku hadi siku. Baada ya kuona hali hiyo akaamua kutafuta
ufumbuzi wa tatizo lake.
Ndipo akakutana na mwanasayansi aliyefanya
kazi katika maabara moja hapo mjini.Mwanasayansi huyu akampa mbinu ya
kuyajaza maputo yale kwa hewa(Hydrogen) ambayo ni nyepesi kuliko hewa
hii ya kawaida(Oxygen) tuivutayo katika miili yetu.
Mfanyabiashara
yule akafanya kama alivyo shauriwa na mwanasayansi, kuyajaza maputo
hewa ya hydrogen, kwa maana hiyo yakawa.
Umewahi kujiuliza kwanini
watu,au kampuni,nchi nyingine zina mafanikio kuliko nyingine? hii
siyo siri,hawa watu wanafikiri na kufanya kazi vizuri,wamejifunza
jinsi ya kuwekeza kwa watu wenye mitazamo chanya.
Mafanikio ya
mtu,kampuni au nchi yanategemea sana ubora wa watu wake.Hivyo
umeona kuwa ni jinsi gani mtazamo ni msingi wa mafanikio.
Mfano kuna jengo moja huko
Marekani lenye urefu wa mita 190.8,lia uzito wa tani 10,884.Ambapo
tani 6,349 iko chini ya ardhi ambayo ni sawa na asilimia 60% ya jengo
zima.Hii ina maanisha na kuoyesha kwamba majengo marefu duniani yana
misingi imara hata karibia robo tatu ya jengo zima.
Kama iliyo kwa jengo refu
na zuri duniani lilivyo na msingi imara,vivyo hivyo hata wewe
unapaswa kuwa na msingi imara.Na huo msingi imara kwa kila binadamu
ni MTIZAMO.
Yuko mkulima mmoja wa
Afrika alikuwa na shamba kubwa analilima na bado alikuwa na maisha
duni siku moja akaja mtu mwenye busara nyumbani kwake akamuambia kuwa
iwapo mkulima huyo angepata almasi yenye ukubwa sawa na kichwa chake
angekuwa tajiri wa kutupwa mpaka kufa kwake yeye na watoto wake
pamoja na wajukuu.
Mkulima huyo aliposikia hivyo haikupita muda akauza
shamba lake lote akasafiri kwenda nchi za nje yeye na familia yake
kwenda kuitafuta almasi na kuinunua alipofika huko akakuta pesa
aliyokuwa nayo ni ndogo haiwezi kununua almasi na alishaitumia kama
nusu hivi kwa gharama za kusafiria mtu huyo kwa presha na mawazo
akaamua kujinyonga akaona kuwa hapo alipofika hawezi kusonga mbele
wala kurudi nyuma shamba na nyumba alishaviuza.
Baada ya muda mfupi yule
mtu aliyeuziwa lile shamba akagundua kuwa kwenye shamba lile kulikuwa
na mawe yanayong`aa akayachukua kwenda kupima akakuta ni almasi
akayauza na kuwa tajiri,yule mtu mwenye busara aliposikia habari hizo
akaamua kwenda kumtembelea yule mkulima alipofika kwenye lile shamba
akamuulizia akaambiwa kuwa mkulima huyo alishaliuza shamba hilo kwa
mtu mingine na akasafiri kuelekea mbali,yule mtu mwenye busara
akasikitika sana.
Stori hii ya mkulima ina
maana kuu tatu : 1.Mtazamo wako unapokuwa sawa,utagundua kwamba
unatembea kwenye mafungu makubwa makubwa ya almasi yaani fursa
(opportunity) ziko chini ya miguu yetu hivyo hatuhitaji kwenda popote
kinachotakiwa ni ugundua nafasi hizo,unaweza ukafa ujaziona almasi
hizo kinaweza kikawa kipaji kila mtu amezaliwa nacho tatizo ni
kugundua kipaji hicho.
2.Majani ya upande wa pili
{shamba la mwenzako} siku zote huonekana ni ya kijani zaidi kuliko
ya shamba lako,wakati unaposifia uzuri wa majani ya upande wa watu
wengine ujue kuna watu wengi wanayakubali majani yaliyopo upande wako
na wanatamani hata kufaya kazi na wewe.Lakini kwasababu hauzingatii
majani ya shamba lako unachukua muda mwingi kuangalia majani ya
shamba la mwenzako hivyo unaweza kufa masikini usipokuwa makini.
Maana ya tatu 3.Bahati
haiji mara mbili kwenye maisha inayofuata inaweza ikawa nzuri zaidi
au mbaya,lakini kamwe haiwezi kujirudia tambua hilo watu wengi
wanashindwa kutamua bahati zao na fursa hata itakapobisha hodi ama
kuonyesha dalili,hata zinapotokea watu wengine huchukulia kuwa ni
jambo la kawaida linapodumu wa muda na kutoweka ndipo wanagundua kuwa
ilikuwa ni bahati ama fursa kama aliitumia vibaya anaanza
kujuta.Maneno mabaya katika maisha ni "ningejua" tatizo
hapa ni kukosa mtizamo.
No comments:
Post a Comment