USIUE NDOTO YAKO KWASABABU YA PESA
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kila mtu
duniani ana ndoto haijalishi ni ndoto gani unayo ,ndoto uliyonayo ina thamani
kubwa kuliko fedha kuliko kitu chochote kile,Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya
kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya
pale ulipotarajia kufika.
Ndoto yako
inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si
kwa
sababu una fedha sana ni kwa sababu una ndoto ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa sana kuliko fedha.
sababu una fedha sana ni kwa sababu una ndoto ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa sana kuliko fedha.
Ndoto
inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda ya ndoto zako yanaweza kuwa fedha ila fedha haiwezi kuzaa ndoto hivyo ndoto ni kubwa kuliko fedha.
Mtu mmoja
aliwahi kusema kuwa mtu masikini kuliko wote duniani ni Yule asiyekuwa na ndoto
hivyo utakubaliana nae kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si masikini tena
maana ana kitu cha thamani na cha pekee na cha tofauti ambacho hamna mwenye nacho usipokua wewe.
Tatizo kubwa
ni kwamba watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha iwe kidogo au kubwa maana hakuna pesa inayozidi ndoto ila ndoto
zinazidi fedha.
Tatizo lingine
ni watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao
kijamii,kiuchumi ,kisiasa na kila Nyanja ya maisha kulingana na ndoto yao
ilivyo .
Ndani ya
ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka kuna kila kitu unachokihitaji iwe ni
fedha ,utajiri,umaarufu,familia nzuri,mume mzuri ,mke mzuri,watoto wazuri,kazi
nzuri,afya nzuri ivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako
utapata kila kitu unachokitaka ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo ,peace of
mind.
Tatizo lipo
kwenye kufanya ndoto zako zitokee ziwe katika uhalisia zikuzalie
mafanikio,haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani kama hautaitimiza ikaja kwenye
uhalisia ikakuzalia mafanikio uwe na uhakika utakufa masikini ukiwa na utajiri
wa ndoto jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaishi
maisha ya chini ya kiwango ambacho walitakiwa kuishi kulingana na ndoto zao.
Kiwango cha
maisha unayoishi kinatakiwa kilingane na kiwango cha ndoto uliyonayo
haiwezekani una ndoto kubwa alafu unaishi maisha madogo ,inasikitisha .Ndoto
yako ndo imebeba kusudi la maisha yako kama utaishi katika ndoto yako maana
yake utakua hujaishi maisha yako maana maisha yako halisi yako kwenye ndoto
zako.
Mtu mmoja
aliwahi kusema kuwa watu wengi duniania hawaishi bali wapo kunatofauti kati ya
kuishi na kuwepo,kuishi ni kutimiza ndoto zako na kuishi ndani ya kusudi la
maisha yako ila kama hautimizi ndoto zako uko nje ya kusudi la maisha yako
maana yake wewe hauishi bali upo ,ama upo upo kama uliwahi kusikia mtu anauliza
vp mzima wewe anajibu mimi nipo nipo yani ni kama ananing`nia angani hana
anachosimamia hana anachotazamia anaishi kama bendera fata upepo .
Anaamka
asubuhi kwa sababu watu wanaamka ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa
sababu watu wameamka hana sababu za msingi,kataa kuishi bila agenda ,bila kuwa
na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika
kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.
Kila kitu kipo
kwenye ndoto zako tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha na kuacha
ndoto zako kwa sababu pesa ni moja kati ya bidhaa iliyoko ndani ya ndoto zako.
Sisemi watu wasitafute pesa wazitafute tena kwa bidii ila wasisahau kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia pesa
zao kama moja kati ya nyezo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao maana hata
maandiko yanasema kuwa pesa ni nguvu.
Ukweli ni kwamba pesa sio kila kitu
pesa huwa hazitoshi na zinaweza zisitosheleze hata kama ni nyingi kiasi gani
kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika lakini katika kutimiza
ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi Fulani (satisfication) hata
kama si kwa asilimia 100% .
Mwandishi Mashuhuri wa Vitabu Myles
Munroe aliwahi kusema kuwa “Watu wenye kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale
ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia zinawasumbua”
“Most frasturated people are these
people who they are dream are not come to the reality” Myles Munroe
Inawezekana unasumbuka sana kwenye
maisha yako kwasababu hujatimiza ndoto zako maana ndoto huwa haimwachi mtu
akatulia inampa mahangaiko,mfadhaiko wa kutaifuta kuiachilia iyo ndoto iliyoko
ndani yako inataka kutokea kwenye uhalisia duniani kwa faida yako na jamii
yako.
Kuwa na ndoto ni kama ujauzito ambao
kila mtu anakua nao haijalishi ni
mwanamke au mwanamke na anatakiwa azae icho kitu kilichoko ndani yake iwe ni kipaji
cha mziki mzuri,vitabu,ubunifu na uwezo Fulani
uje kwe uhalisia.
Hivyo kila mtu anapaswa azae ,ndoto
yako izae ,uwezo ulionao uzae unaweza kukuzalia mafanikio makubwa usikubali
kufa na kitu cha tahamani kilichoko ndani yako kilete duniani kitoe kilete
mabadilko .
Hakuna ndoto kubwa wala ndoto ndogo
fikiria mtu aliyegundua lipstick mafuta ya kupaka mdomoni leo hii wanawake
dunia nzima wanapaka lipstick si jambo dogo hata kidogo.
Hujaja duniani kuwa mtu wa
kuhangaikia fedha ,inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe ,pesa ikupende na
ikutamani na si wewe utamani fedha maana tamaa ya fedha ni mbaya inazaa uovu na
uasi wakati mwingine.
Tengeneza miundombinu ya pesa
kukufikia na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako ,maono yako,kipaji chako na uwezo
ulionao.
Kwenye ndoto zako Kuna ramani na barabara za watu
kupita kukuletea fedha kutokana na kile ulichonacho,kile ulichonacho ni cha
thamani sana.
Kile ulichonacho ni kikubwa zaidi ya
fedha ,tafuta kukitimiza hicho ulichonacho ,anza sasa uwezo unao nguvu unayo.
Katika kutimiza ndoto zako usikubali
kuzuiwa na fedha,mazingira ,mtazamo hasi,marafiki,jaribu kuwa mtu asiyezuilika
ili uweze kuzifikia ndoto zako.
0765938008
No comments:
Post a Comment