FURSA UNAZOWEZA KUTENGENEZEA
KIZAZI CHAKO KWA WEMA UNAOUTENDA LEO
Na Samuel Sasali
Wema Ni Akiba, Wema Hauozi... Mara nyingi sana ni rahisi
kumfanyia wema yule ambaye amekufanyia wema ama una amini anaweza kukufanyia
wema hapo baadae. Ni nadra sana kutenda wema kwa mtu aliyewahi kukutendea uovu
ama ubaya ama ambaye unaamini atakufanyia ndivyo sivyo.
Wema ni akiba kubwa sana katika maisha. Hakuna aliyepata thawabu
kwa kuwafanyia wema wale ambao humfanyia wema. Watu ambao hawakutarajiwa
kufanya wema wakifanya wema ama wakifanyiwa wema hugeuka kuwa jambo la
kujifunza. mwisho wa siku Asiyetarajiwa ndiye hutenda wema.
Huwezi jua unayemsaidia leo kwenye maisha atakuja kuwa nani. Na
usifanye wema ukitarajia kwamba pia utatendewa wema. Tenda wema nenda zako.
Wema ni akiba nzuri sana. Mara kadhaa nimewahi kutana ambao wamefaidi wema
uliofanywa na Wazazi wao.
Kuna fursa utawatengenezea kizazi chako kwa wema unaoutenda leo.
Usitende ubaya wakati una uwezo wa kutenda wema. Usinyanyase wengine kwa sababu
ya NAFASI uliyonayo leo.
Cheo ni dhamana. Wema wako
ni akiba isiyooza. Huwezi jua watu wangapi wanafaidika na kunufaika kwa kile
unachokifanya hata kama hakuna anayekuambua.
Kuna tofauti ndogo sana ya Kutenda wema na Kutafuta Sifa.
Usifanye kitu ili uonekane watu wakukubali. Ukitenda wema ni mbegu isiyokufa
hata kama katika wakati wa uhai wako haitachipua.
Kuna fursa kadhaa nimepata kwa sababu ya Wema wa Wazazi wangu kwa
watu Kadhaa. Kwenye Harusi yangu nilipata Support kubwa pia sababu Wazazi wangu
waliwekeza kwenye Maisha ya Watu. Nini unawekeza kwenye maisha ya watu na
kwafaida ya nani.
Wema ni akiba isiyooza, kwa kutenda wema tunawapalia makaa ya
hatia wale waliodhani hatutawatendea wema. Hakuna funzo lolote linapatikana kwa
kutenda wema kwa mtu aliyekutarajia.
No comments:
Post a Comment