Thursday 15 October 2015

Misukosuko ndiyo chachu ya maendeleo ya ndoto zetu.



Misukosuko ndiyo chachu ya maendeleo ya ndoto zetu.

Na Samuel Sasali

Ukweli ni kwamba Viwanja vya ndege kuna mazingira mazuri kuliko angani lakini ndege hazijaumbwa zikae airport, kinachotofautisha gari na ndege ni anga.

 Angani kuna misukosuko lakini ndoio ndege zimetengenezewa mazingira thabiti. Hata kama Bandarini ni pazuri namna gani lakini ukweli ni kwamba Meli na Boti zimeumbiwa majini.

Hapo ulipo inawezekana ni kiwanja cha ndege ama bandarini ambapo kiukweli ni pazuri sababu hapana misukosuko lakini kumbuka ili ndege itoke destination moja kwenda nyingine kuna dhoruba kadhaa itakumbana nazo.


Ili uweze kuvuka na kufika hatma ya maisha yako ni lazima utoke hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine. Misukosuko ni jambo la kawaida.

Bandarini ama airport uliyopo imekusababishia kujisahau na ku relux na kujisahau.


Tambua kuwa usipoamua kupiga hatua hakuna siku utapiga hatua.


Ukibadilika Mazingira yatabadilika na Hatma yako itabadilika.


 




No comments:

Post a Comment